pmbet

Hamisa Mobetto ampiga chini Wema Sepetu Instagram.

Joyce Shedrack

June 21, 2024
Share :

Mwanamitindo na msanii wa muziki Hamisa Mobetto amekuwa mwanamke wa kwanza Tanzania kuwa na wafuasi wengi kwenye mtandao wake wa Instagram baada ya kufikisha wafuasi milioni 11 na laki tano.

 

Mrembo huyo ambaye ni balozi wa PMBET ameweka rekodi hiyo baada ya kumfikia na kumpita  Miss Tanzania wa mwaka 2006 na mwigizaji maarufu Wema Sepetu ambaye mpaka sasa ana wafuasi milioni 11 na laki tano kwenye mtandao wa instagram.

 

Hamisa alianza kujipatia umaarufu baada ya kugombea Miss Tanzania mwaka 2011 na kuishia hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo kabla ya kugeukia sanaa ya maigizo iliyomtambulisha zaidi na badae kujiingiza kwenye sanaa ya muziki kwa kuwa mwimbaji wa bongofleva.

 

Hivi karibuni Hamisa amejikita zaidi kwenye biashara zake binafsi na kulea watoto wake huku akipunguza nguvu kwenye sanaa zilizomtambulisha jambo ambalo mpaka sasa watu wengi wanashangaa kwa umaarufu anaoendelea kuupata. 

 

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet