pmbet

Hamisa na Aziz Ki ni wanandoa kwa miezi minne sasa.

Joyce Shedrack

February 11, 2025
Share :

Mwanamitindo maarufu na msanii wa Tanzania Hamisa Mobetto amefunga ndoa na mpenzi wake ambaye ni mchezaji wa Yanga raia wa Burkina Faso Stephane Azizi Ki miezi minne iliyopita hivyo ni mume na mke na siyo wapenzi kama watu wengi wanavyofahamu.

Mama Mzazi wa Hamisa Mobetto maarufu kama Mama Mobetto amethitibisha hii leo kupitia kipindi cha leo tena cha Clouds Fm na kusema kwamba kinachoenda kufanyika hivi karibuni ni sherehe tu lakini ndoa tayari ilifungwa miezi minne iliyopita.

 

“Aziz na Hamisa ni mke na mume muda mrefu walikuja wawakilishi wachache kutoka kwenye familia yake siku ya ndoa na wawakilishi wa GSM” amesema Mama Mobetto.

 

Ikumbukwe,Wawili wamekuwa kwenye mahusiano ya siri kwa muda mrefu kabla ya siku chache kuamua kuweka penzi lao hadharani kufuatia picha walizozichapisha kwenye kurasa zao za Instagram.

 

Sherehe za ndoa yao zitafanyika rasmi tarehe 19 mwezi huu huku tarehe 15 ikiwa ni siku ya mahari na tarehe 16 itakuwa ni siku ya Nikkah.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet