"Hamna wachezaji wenye uwezo wa kuifunga Man City" Scholes awachana Man U!
Eric Buyanza
March 4, 2024
Share :
Gwiji wa Manchester United, Paul Scholes amewashambulia Mashetani Wekundu kufuatia kipigo ilichokipata cha mabao 3-1 kutoka kwa Manchester City Jumapili.
Baada ya mchezo huo Scholes amekaririwa akisema Man United haina wachezaji wenye uwezo wa kuifunga Man City kwa sasa.
Akizungumza na Premier League Productions, Scholes alisema:
“Pengine ni matokeo sahihi....Kwa muda huu Man City iko kwenye viwango vya juu.....Man United hawana wachezaji kwa sasa ambao wana uwezo wa kuifunga."