Hamuogopi...? Halland afikisha hat-trick 18 akiwa na miaka 23
Sisti Herman
February 28, 2024
Share :
Baada ya kufunga magoli matano dhidi ya Luton Town kwenye mchezo wa kombe la FA wakishinda 6-2, mshambuliaji wa Manchester City Erling Haaland tayari amefikisha hat-tricks (mabao matatu kila mechi) 18 katika mashindano nane tofauti tangu aanze kucheza timu za wakubwa.
Ligi kuu Uingereza (Premier League) - 5
Ligi kuu Ujerumani (Bundesliga) -3
Ligi kuu Austria (Bundesliga) - 3
Ligi ya mabingwa Ulaya (Champions League) - 2
Kombe la FA Uingereza - 2
Kombe la FA Austria - 1
OFB Cup - 1
Kombe la FA Ujerumani (DFB-Pokal) - 1
Mshambuliaji huyo ndiyo kwanza ana miaka 23, Je uaona akifika wapi?