pmbet

Hans Flick amuomba radhi Xavi Hernandez kisa Barcelona.

Joyce Shedrack

March 9, 2026
Share :

Kocha wa zamani wa Barcelona Xavi Hernández amefunguka kwamba kocha wa sasa wa Barcelona Hans Flick alienda nyumbani kwake kumuomba radhi baada ya kumficha kuwa alikuwa kwenye mazungumzo ya kujiunga na timu hiyo wakati yeye akiwa bado ni kocha mkuu. 

Xavi Hernández Surprises Hansi Flick with an Unexpected Call and This  Message

Xavi ameweka wazi kuwa viongozi wa klabu ya Barcelona walikuwa wanafanya mazungumzo na Hansi Flick huku wakati huo huo wakimwaminisha kuwa yeye angebaki kuwa kocha wa timu hiyo.

 

“Hansi Flick alikuja kuniomba radhi nilipomuuliza kama kweli klabu ilikuwa imekuwa ikizungumza naye wakati mimi bado nilikuwa kocha...”

 

“Katika zile wiki 2 au 3 ambazo klabu ilikuwa tayari imeamua kuniondoa lakini hakuna aliyeniambia moja kwa moja.” 

 

“Flick aliomba radhi, tukazungumza kwa zaidi ya saa mbili, ilikuwa mazungumzo mazuri sana. Klabu ilikuwa imemwambia asiniambie chochote, na ndiyo maana alikuja nyumbani kwangu kuniomba radhi.” 

 

“Yeye ni mtu mzuri, mwenye heshima na moyo wa uadilifu, na ninafurahi mambo yanamwendea vizuri.”Amesema Xavi 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet