Hapatatoshi kesho, Arsenal kuvaana na Man City kufungua msimu
Eric Buyanza
August 15, 2026
Share :

Arsenal inaingia dimbani dhidi ya Manchester City kesho Agosti 16, 2026 kwenye mchezo wa fainali ya Ngao ya Jamii. Huu ni mchezo maalum unaofungua msimu mpya wa soka nchini Uingereza.
Ikumbukwe kuwa Arsenal ataingia kama bingwa wa Ligi Kuu (Premier League) na Manchester City kama bingwa wa Kombe la FA.
Kikosi cha Mikel Arteta kilianza maandalizi ya msimu kwa ushindi mzuri dhidi ya MK Dons na Girona, kabla ya kupata vipigo kutoka kwa Real Betis na Borussia Dortmund.
Hata hivyo wamekuwa na utulivu katika kipindi hiki cha kiangazi, huku usajili wa Bruno Guimaraes ukiwapa nguvu zaidi baada ya kuimarisha safu yao ya kiungo.
Iwapo Arsenal wataifunga Manchester City, ambayo inaanza enzi mpya baada ya kuondoka kwa Pep Guardiola, ushindi huo utakuwa ujumbe kwamba bado ni moja ya timu zinazopaswa kuogopwa na wapinzani wao katika mbio za ubingwa.
Arsenal wataingia msimu huu wakilenga kutetea taji lao, huku ushindi dhidi ya Manchester City ukiweza kuwa mwanzo muhimu wa safari hiyo.





