Harmonize aachia ngoma mpya ya mpya ya Yanga.
Joyce Shedrack
August 1, 2024
Share :
Mwimbaji staa wa Bongofleva Harmonize ametambulisha rasmi wimbo wake mpya wa hamasa aliouimba maalum kwa ajili ya Yanga ambao atautumbuiza siku ya wananchi Jumapili ya weekend hii.
“Ifike wakati Msanii ukipata nafasi ya kuperfom kwenye jukwaa kama hili kwangu ni kitu kikubwa ni zaidi ya super bowl kwahiyo ni mara ya pili kuperfom na nimejiandaa sitaki niongee sana safari hii nataka nioneshe vitendo zaidi, kwangu hii ni Yanga Day bora”-Harmonize.
Sambamba na hilo Msemaji wa klabu hiyo Haji Manara amesema wanaenda kuujaza uwanja huo kiukweli sio kama walivyofanya watani wao Simba Sc kwa kugawana tiketi kwa mafungu (akitumia neno ulanguzi).
Manara amesisitiza kuwa wao hawafanyi biashara ya ulanguzi na ukweli utathibitika siku ya tukio kwa uhalisia kuonekana wa nani atakayejaza uwanja huo wa Benjamini Mkapa.
Ikumbukwe, Siku ya jana klabu ya Simba ilitangaza kumaliza kuuza tiketi zote za sherehe ya siku ya Simba Day ikiwa ni siku tatu kabla ya kufika siku yenyewe huku Yanga ambao walianza kuuza tiketi mapema zaidi kabla ya watani zao tiketi zao zikiendelea kusalia sokoni huku wakitangaza kumaliza tiketi za VVIP na VIP A pekee.
Tamasha la Simba Day litafanyika jumamosi ya tarehe 3 mwezi huu huku Wananchi wakisherekea kilele cha wiki yao tarerhe 4 siku ya jumapili.