Harmonize kutambulisha wasanii wapya wawili kwenye lebo yake.
Joyce Shedrack
July 16, 2025
Share :
Staa wa Bongo Fleva na Mmiliki wa Konde Music Harmonize ametangaza kutambulisha wasanii wapya wawili kwenye lebo yake ya Konde Music kabla ya mwaka mwaka kuisha.
Harmonize ametoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram wakati akiwashukuru mashabiki baada ya akaunti ya Instagram ya Konde Music kufikisha wafuasi milioni tatu.
"Unajua nini kuna nyimbo mbili zinakuja kabla ya Agosti mwaka huu, na kama haitoshi kuna wasanii wawili wanakuja mwisho wa mwaka huu," ameandika Harmonize.