Harry Kane afichua alivyocheza gofu na Rais Trump
Eric Buyanza
July 11, 2026
Share :
Nahodha wa timu ya taifa ya England, Harry Kane, amesema alicheza gofu na Rais wa Marekani, Donald Trump, takribani miezi 18 iliyopita huko Palm Beach, Florida, na kueleza kuvutiwa na kiwango cha uchezaji wa Trump licha ya umri wake mkubwa wa miaka 80.
Kane alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa robo fainali ya Kombe la Dunia, ambapo England inashuka dhidi ya Norway, leo Jumamosi.






