Harry Kane avunja rekodi ya Rooney EURO
Sisti Herman
July 11, 2024
Share :
Baada ya jana kufunga goli kwenye ushindi wa 2-1 dhidi ya Uholanzi kwenye mchezo wa nusu fainali ya kombe la Mataifa Ulaya (EURO), Nahodha na mshambuliaji kinara wa timu ya Taifa Uingereza Harry Kane jana amefanikiwa kuvunja rekodi ya kuwa mchezaji wa Uingereza mwenye magoli mengi kwenye michuano hiyo kwa kufikisha magoli 7.
Rekodi hiyo kabla ilikuwa ikishikiliwa na aliyekuwa Nahodha na Mshambuliaji kinara wa nchi hiyo Wyne Rooney aliyekuwa na magoli 6.
Baada ya ushindi huo ambao ulikamilishwa na goli la Ole Watkins, Uingereza imefanikiwa kuingia fainali na itacheza dhidi ya Hispania waliowaondoa Ufaransa, fainali itapigwa Julai 14.