Harry Kane ndiye mwanaume anayestahili Ballon D'or 2026 – Ferdinand
Eric Buyanza
August 24, 2026
Share :

Beki wa zamani wa Manchester United, Rio Ferdinand, amedai kuwa hakuna mchezaji mwingine anayestahili tuzo ya Ballon d'Or 2026 zaidi ya Harry Kane.
Ferdinand alitoa kauli hiyo wakati akimpongeza nahodha huyo wa Uingereza baada ya kukabidhiwa tuzo ya Kiatu cha Dhahabu cha Ulaya (European Golden Shoe).
Kwa mujibu wa Ferdinand, takwimu za ufungaji mabao za mshambuliaji huyo wa Bayern Munich zinamfanya kuwa mgombea wa pekee asiye na mpinzani.
"Mabao 73 kwenye msimu mmoja; ni Lionel Messi pekee aliyewahi kufunga mabao mengi zaidi katika msimu mmoja kuliko Harry Kane. Umeshinda Kiatu cha Dhahabu cha Ulaya, ukiwa mfungaji bora wa Uingereza kwenye Kombe la Dunia. Nani mwingine? Nani mwingine anayepaswa kushinda Ballon d'Or zaidi ya Harry Kane? Kuna mtu mmoja tu, Harry Kane," alisema Ferdinand,





