pmbet

Harusi ya Cristiano Ronaldo kugharimu zaidi ya Bilioni 30

Eric Buyanza

August 5, 2026
Share :

Cristiano Ronaldo, nyota wa zamani wa Manchester United, Real Madrid na Juventus, anatarajiwa kufunga ndoa wikendi hii.

 

Mwanasoka huyo raia wa Ureno atamuoa mpenzi wake wa muda mrefu, Georgina Rodriguez, tarehe 8 Agosti katika kisiwa cha Madeira, kama ilivyoripotiwa na gazeti la The Sun la Uingereza.

 

Kwa mujibu wa The Sun, wawili hao wamechagua kufanyia harusi yao mjini Funchal, makao makuu ya kisiwa hicho, ambacho Ronaldo alikulia akiwa mtoto.
 

Baada ya kanisani, tafrija kubwa (reception) itafanyika kwenye hoteli ya kifahari ya nyota tano 'Savoy Palace' ambapo ghorofa kadhaa na kumbi za hoteli hiyo zitafungwa maalum kwa ajili ya ulinzi na faragha ya wageni kwa siku ya Jumamosi na Jumapili.
 

Inakadiriwa kuwa harusi hii itagharimu zaidi ya shilingi bilioni 30 za Kitanzania, na kuifanya kuwa moja ya harusi ghali zaidi za mastaa duniani.

 

Kwenye harusi hii tunategemea kuona mchanganyiko wa wageni mashuhuri (VIP) kutoka sekta mbalimbali duniani.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet