Harusi ya Manara kujaza uwanja wa Mkapa
Sisti Herman
January 30, 2024
Share :
Baada ya kufunga ndoa na mwigizaji wa tamthilia Zaylissa, aliyekuwa msemaji wa klabu kubwa za soka nchini Simba na Yanga, Haji Sunday Manara kupitia shapisho la mtandao wake wa kijamii wa instagram amedokeza kwa kuuhusisha uwanja wa Benjamin Mkapa na harusi yake.
Manara ameandika “Ni kwa Mkapa. De Grand Royal Wedding Party au tukafanyie angani na Dreamliner ya ATC mkaturoge kisha ndege ianguke?”
Kwa uzoefu wake wa kuhamasisha na kujaza uwanja akiwa msemaji wa Simba na Yanga, Je harusi yake itaweza kujaza uwanja? tupe maoni yako kwenye comment