pmbet

Hasira kila mahali Kenya kisa kukatika umeme masaa 4!

Eric Buyanza

December 12, 2023
Share :

Desemba 10, 2023 Umeme ulikatika mara tatu kwa takriban saa nne mfululizo hali iliyosababisha Raia kupata gadhabu na kutoa malalamiko juu ya utendaji kazi wa Kampuni ya Umeme ya Kenya Power.
 

Sehemu zilizoathirika ni pamoja na Kisumu, Mombasa, Saba Saba, Bomet, Tana River, Nanyuki, Kakamega, Lamu, Murang’a, Nakuru, Makueni, Tharaka-Nithi, na Machakos.
 

Wananchi wameonesha ghadhabu zao mitandaoni wakimtaka Waziri wa Nishati ajiuzulu na kumshinikiza Rais Ruto kufanya mabadiliko katika sekta hiyo huku Kenya Power ikidai shida ilitokana na hitilafu kwenye Mitambo.
 

Hali hiyo iliathiri shughuli mbalimbali ikiwemo huduma za Treni ya Kisasa, (SGR), na Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta na kufanya Wananchi kudai kuwa Kenya ni nchi pekee ambayo Umeme unakatika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet