'Hat-Trick' ya Mbappe yaipeleka Madrid 16 bora Ligi ya Mabingwa Ulaya
Eric Buyanza
February 20, 2025
Share :
Mabao ya "Hat-Trick" yaliyofungwa na mshambuliaji wa Real Madrid Kylian Mbappe, yamekifanya kikosi hicho kuingia kwenye 16 bora ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuwabwaga vibaya Manchester City ya England kwa mabao 3-1.
Kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita, Madrid ilitoka kifua mbele kwa mabao 3-2 na kuwaondosha wababe hao wa Ligi ya Premier kwa jumla ya mabao 6-3.
Akiongea na tovuti ya UEFA baada ya mchezo huo, Mbappe alisema kwao kama timu ulikuwa ni usiku mzuri sana kwao, kwa kuwa walichokuwa wakikihitaji ni kusonnga mbele.
Mbali na mechi hiyo, PSG nayo imechupa kwenye 16 bora baada ya kuirarua Brest kwa mabao 7-0, huku Juve ikitolewa na PSV Eindhoven baada ya kipigo cha 3-1, huku Borrusia Dortmund nayo ikifuzu baada ya sare ya bila kufungana na Sporting Lisbon.