Hata kukaa uc...i ni sanaa - Fid Q
Eric Buyanza
December 5, 2023
Share :
Kwenye swala zima la kuelezea sanaa, kila mtu ataielezea kwa jinsi anavyoijua, lakini kwa upande wa nguli wa muziki wa Hiphop nchini, Fid Q anasema hata kukaa uchi ni sanaa.
Katika kulielezea hilo kwa mapana, Fid Q anasema kukaa uchi huko kutategemea mkaaji alikaa uchi wapi na saa ngapi?
"Ukikaa uchi saa 7 mchana tena Kariakoo, hapo utakuwa umejiletea shida......lakini ukiwa hivyo saa 7 mchana umejifungia ndani kwako na watu wazima wenzako na mna vitu vyenu vinaendelea, hiyo ni sanaa" anasema Fid Q.
Anasisitiza watu watofautishe kukaa uchi na kufanya mat**i kwasababu hivyo ni vitu viwili tofauti.
Kwa mujibu wa Fid, mwili wa binadamu ulivyo....uwe na kitambi au six pack hiyo ni sanaa, na msanii namba moja duniani ni MUNGU.
Fuatilia hiyo video hapo chini.