“Hata nikistaafu leo, bado hautakuwa kwenye kiwango changu” – Wizkid amwambia Davido
Eric Buyanza
April 30, 2024
Share :
Nyota wa muziki wa AfroBeat kutoka Nigeria, Ayodeji Balogun, almaarufu Wizkid, amejigamba kuwa hata akiamua kustaafu muziki leo, bado Davido hatakuwa kwenye kiwango kama chake.
Wizkid alisema hayo jana Jumatatu wakati wa majibizano makali na Davido kwenye mtandao wa kijamii wa X (zamani Twitter) huku akimuita Davido 'Bwana mdogo'.