Hatari sana, kiuno cha 'Malaika Cute' kimebeba cheni za milioni 14
Eric Buyanza
August 9, 2024
Share :

Malaika Cute, aliyewahi kuwa mke wa mtangazaji wa Wasafi FM, Ricard Momo, ameongea na waandishi wa habari na kuweka wazi kuwa cheni alizovaa kwenye kiuno chake kwa ujumla zina thamani ya shilingi milioni kumi na nne na laki nane (14.8 Million).
Kwa mujibu wa Malaika, kwenye kiuno chake kuna cheni tatu, ya kwanza ya dhahabu ina thamani ya shilingi milioni 9, ikifuatiwa na ya milioni 4 na ya mwisho ina thamani ya shilingi milioni 1.8...tukijumlisha zote tunapata milioni 14.8 (Jumla).
Tazama video hapo chini





