pmbet

Hatimae Joseph Kabila arejea Kongo, atembelea mji wa Goma

Eric Buyanza

April 19, 2025
Share :

Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Joseph Kabila, amewasili katika mji wa Goma siku chache tu baada ya kutangaza kuwa atarejea nyumbani kupitia eneo la mashariki mwa nchi hiyo.

Ripoti zinaonyesha kuwa Kabila, ambaye alikuwa akiishi Afrika Kusini, aliwasili Goma Ijumaa mchana na aliingia nchini humo akipitia Rwanda.

Tangu kuondoka madarakani, Kabila ametumia muda wake mwingi nchini Afrika Kusini, ingawa pia ameishi Zimbabwe.

Taarifa za kurejea kwa Kabila nchini DRC zilianza kusambaa mapema mwezi huu, huku vyanzo vikifichua kuwa maandalizi ya kumkaribisha yalikuwa yakiendelea kwa siku kadhaa.

Kabila bado anabakia kuwa mtu mwenye nguvu na ushawishi mkubwa kwenye siasa za Kongo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet