pmbet

Hatimae Mahakama yamruhusu Jacob Zuma kugombea Urais

Eric Buyanza

April 10, 2024
Share :

Mahakama nchini Afrika Kusini jana Jumanne ilitoa maamuzi ya kumruhusu aliyekuwa Rais wa zamani Jacob Zuma kugombea urais kwenye uchaguzi mkuu ujao, na hivyo kubatilisha uamuzi uliotangazwa na tume ya uchaguzi wiki iliyopita wa kumzuia kugombea. 

Katika hali ambayo wengi hawakuteigemewa, mahakama ya uchaguzi ilimpa haki rais huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 81, ambaye atawania kwa tiketi ya chama cha uMkhonto we Sizwe (MK), chama kipya cha upinzani ambacho kinaonekana kuwa tishio kwenye uchaguzi wa Mei 29. 

Uchaguzi mkuu wa nchi hiyo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa na kuwepo kwa Zuma katika kiny'ang'anyiro inaweza kuwa kichocheo cha ushindani huo. 

Kikitegemea umaarufu wa Zuma, chama cha MK kinatarajiwa kugawana kura na chama tawala cha African National Congress. Hiyo inaweza kupelekea kura za ANC kushuka chini ya asilimia 50 kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1994.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet