pmbet

Hatimaye Bayer Leverkusen wamepoteza msimu huu

Sisti Herman

May 23, 2024
Share :

Baada ya kuwa na msimu bora na kushuhudiwa kutopoteza mchezo wowote kwenye mashindano yote hatimaye klabu ya Bayer Levekursen imepoteza mchezo wake wa kwanza msimu huu dhidi ya Atlanta kwenye mchezo wa fainali ya kombe la ligi ya Ulaya (Europa League).

Levekursen inayofundishwa na kocha kijana Xabi Alonso ilicheza michezo 51 kwenye mashindano yote waliyoshiriki msimu huu kama Bundesliga ambayo walitwaa taji bila kufungwa, Europa League ambayo walifungwa jana fainali na DFB Pokal ambayo wapo hatua ya fainali.

Hadi sasa Levekursen msimu huu;

- Wamecheza mechi 52
- Wameshinda mechi 42
- Sare 9
- Wamefungwa mechi 1

Siku ya Jumamosi Levekursen waahitmisha msimu kwa mchezo wa fainali ya kombe la ligi ya Ujerumani (DFB Pokal) dhidi ya Kaiserslautern.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet