Hatimaye Nigeria yaanzisha idhaa ya Kiswahili
Eric Buyanza
July 11, 2024
Share :
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba Chacha amesema ushirikiano ulioanzishwa baina ya TBC na Sauti ya Nigeria (VON) umefanikisha kuanzishwa kwa chombo cha habari kinachotangaza kwa kutumia lugha ya Kiswahili nchini Nigeria.
Dkt. Rioba amesema hayo wakati wa ziara ya Mkurugenzi Mkuu wa VON Jibrin Baba Ndace katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi iliyopo mkoani Morogoro.
“Sisi tumekuwa na ushirikiano na VON ambao wanacho chombo cha habari kinachotangaza lugha ya Kiswahili kabisa na sisi tumepeleka mtu kule ambaye ataripoti taarifa zetu na za kule atazileta huku.” amesema Dkt. Rioba