pmbet

Hatma yake ni Aston Villa aliaga akaondoka dili lingine la kuondoka limekufa.

Joyce Shedrack

August 7, 2026
Share :

Kipa nyota wa Argentina, Emiliano Martínez, amejikuta katika hali isiyo ya kawaida katika maisha yake ya soka ngazi ya klabu licha ya kuwa miongoni mwa makipa bora zaidi duniani.

Emiliano Martinez is shown a straight RED CARD for a bizarre BLOCK on  Rasmus Hojlund as Aston Villa's quest for Champions League football takes a  damaging blow at Manchester United | Daily

Mwisho wa msimu wa 2024/25, Martínez aliondoka uwanjani akiwa na machozi huku akiwaaga mashabiki wa Aston Villa. Wakati huo, ilitarajiwa kwamba angeondoka katika klabu hiyo na kujiunga na moja ya vigogo vya Ulaya, baada ya kuhusishwa na klabu kadhaa kubwa ikiwemo Manchester United.

 

Ripoti zinasema Martínez alikuwa tayari hata kuachana na nafasi ya kucheza michuano ya Ulaya ili kujiunga na Manchester United, na  alimuomba mwenzake wa Argentina, Lisandro Martínez, kusaidia kusukuma uhamisho huo lakini Manchester United ikaamua kumsajili kipa Mbelgiji Senne Lammens, na hivyo mipango ya Martínez kuhamia Old Trafford ukayeyuka.

 

Matokeo yake, Martínez alilazimika kurejea Aston Villa baada ya tayari kuonekana akiwaaga mashabiki wa klabu hiyo.

 

Msimu huu, Juventus walionekana kuwa karibu kumsajili, huku taarifa zikidai kuwa makubaliano binafsi yalikuwa yamefikiwa cha kushangaza dili hilo nalo lilivurugika na hatimaye likafa rasmi baada ya Juventus kuijulisha Aston Villa imesitisha mpango wa kumsajili kipa huyo.

 

Kwa sasa Martínez bado yupo Aston Villa akijiandaa na msimu ujao huku akiwa hajapata ofa ya maana kutoka klabu kubwa za Ulaya.

licha ya kuwa na mafanikio makubwa akiwa na Argentina.

🏆 Kombe la Dunia
🏆 Copa América
🏆 Finalissima
🧤 Golden Glove ya Kombe la Dunia

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet