Hatujadharau Mapinduzi Cup - Ali Kamwe
Sisti Herman
January 8, 2024
Share :
Meneja wa Habari na Mawasiliani Yanga SC, Ally Kamwe akizungumza baada ya klabu hiyo kupoteza mchozo wa robo fainali ya Mapinduzi Cup amesema klabu hiyo haijadharau mashindano hayo na walijipanga kufanya vizuri ila mipango yao haijatimia.
Yanga imepoteza mchezo wa robo fainali kwa kukubali kichapo cha mabao 3-1 kutoka APR ya Rwanda, Kamwe amesema sasa ataishabikia klabu ya Mlandege ambayo imefuzu hatua ya nusu fainali.