Hatumfukuzi kocha bado tuna imani naye
Eric Buyanza
January 22, 2024
Share :
Waziri mwenye dhamana ya michezo nchini Dkt. Damas Ndumbaro ameweka wazi kuwa bado wapo na kocha mkuu Adel Amrouche hadi adhabu yake itakapotamatika kwa sababu ndiye aliyeifikisha timu kwenye michuano ya AFCON hivyo wataendelea kuwa nae na hawatasitisha mkataba wake.
Dkt. Ndumbaro amesema kuwa...
“Bado sisi kama Serikali ambao ndio walipa mshahara ukiadhibiwa sio muda wa kumzodoa, tupo naye kwenye kipindi hiki kigumu anachopitia”.
“Bado tuna imani na mwalimu, yeye ndiye ametufikisha hapa sehemu ya kufuzu, Mwalimu huyu ndiye ametengeneza timu hii, tupo na mwalimu, hatujasitisha mkataba, ameadhibiwa na CAF, hajaadhibiwa na serikali wala TFF”.
“Sisi katika kipindi hiki kigumu ambacho mwalimu ana kipitia tuko nae na tutaendelea kuwa nae, kumpa sapoti yote ambayo inahitajika, ili yeye apite kwenye kipindi hiki kigumu kwa salama kabisa”. Dkt. Ndumbaro Waziri wa utamaduni Sanaa na michezo
Kwasasa Taifa Stars ipo chini ya kocha wa muda Hemed Suleiman ambaye anasaidiwa na kocha wa zamani wa klabu ya Simba Juma Mgunda.
Tarehe 24 mwezi huu Taifa Stars chini ya Hemed Morocco itaenda kutupa karata yake ya mwisho hatua ya makundi dhidi ya DR Congo mchezo utakao amua hatma ya Taifa stars katika michuano hiyo.