Hatuna mpango wowote wa kumsajili Enzo Fernández - Real Madrid
Eric Buyanza
July 4, 2026
Share :

Klabu ya Real Madrid imesisitiza kuwa haina mpango wowote wa kumsajili Enzo Fernández baada ya wakala wa kiungo huyo kufichua kuwa anatafuta njia za kuondoka Chelsea.
Javier Pastore, anayemwakilisha Fernández, hakuthibitisha waziwazi nia ya Madrid, lakini mapema wiki hii alidokeza kulikuwa na uwezekano wa uhamisho kwenda klabu hiyo ya Uhispania .
"Kufuatia taarifa na kauli zilizojitokeza siku za hivi karibuni kuhusu madai ya nia ya kumsajili Fernández, klabu inapenda kueleza kuwa haijafanya jitihada zozote, iwe za moja kwa moja au zisizo za moja kwa moja, zenye lengo la kumsajili mchezaji huyo," Madrid ilisema katika taarifa yake siku ya Ijumaa.
"Aidha, klabu haina mpango wowote wa kufuatilia jambo kama hilo."
Mara nyingi klabu haziwekagi wazi kuhusu habari zao usajili, lakini Madrid iliona ni muhimu kufanya hivyo.





