Hatutafuti vita, lakini pia hatuviogopi -Rrais wa Cuba
Eric Buyanza
July 3, 2026
Share :

Rais wa Cuba, Miguel Díaz-Canel amesema katika mahojiano na Sky News kwamba anachukulia kwa uzito vitisho vya Donald Trump vya uwezekano wa kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Cuba.
Amesema yuko tayari kupigana "hadi tone la mwisho la damu" kwa ajili ya nchi yake na maadili ya jamii ya Cuba.
Katika mahojiano ya kipekee na Sky News siku ya Alhamisi, Díaz-Canel alisema:
“Hatutafuti vita, lakini pia hatuviogopi.”
Kauli za Díaz-Canel zinajibu vitisho vya mara kwa mara vya Donald Trump dhidi ya mji mkuu wa Cuba, Havana, pamoja na taarifa zinazoonesha kuongezeka kwa uwepo wa kijeshi wa Marekani karibu na mipaka ya bahari inayozunguka Cuba.
BBC





