"Hatutaki chochote zaidi ya zawadi yetu ya ubingwa" Andre Mtine.
Joyce Shedrack
June 11, 2025
Share :
Afisa Mtendaji Mkuu wa klabu ya Yanga Andre Mtine amewasili siku ya leo katika ofisi za TFF kwa ajili ya kufuatilia kuhusu madai ya fedha za zawadi ya ubingwa wa kombe la CRDB, kwa msimu uliopita huku akisisitiza kuwa hawana haja ya kujadili masuala mengine yoyote kwa sasa zaidi ya kukamilishwa kwa malipo hayo.

“Sisi hatutaki chochote zaidi ya zawadi yetu ya ubingwa kama kuna jambo lolote watuwasilishie kwa njia ya maandishi ila kwasasa hatuhitaji jambo lolote zaidi ya zawadi yetu ya ubingwa.”
"Wewe umeshawahi kuona wapi Duniani kote hela ya madeni ikakatwa kwenye hela ya zawadi za ubingwa? Kwanza mnajua thamani ya fedha ya bingwa? Na wapi wametangaza thamani ya fedha za ubingwa?."- CEO wa Yanga.