Hatuyataki majeshi ya Israel lebanon - Kiongozi wa Hezbollah
Eric Buyanza
June 22, 2026
Share :

Kiongozi wa Hezbollah, Naim Qassem, alijibu kauli za Waziri Mkuu wa Israel siku ya Jumapili kuhusu majeshi ya Israel kuendelea kubaki katika eneo la usalama kusini mwa Lebanon, akisema:
“Haiwezekani kwa majeshi ya Israel kubaki nchini Lebanon.”
Aliongeza:
"Hakuna eneo la usalama kwa Israel. Tuna jeshi la taifa ambalo lina jukumu la kulinda nchi, na sisi tunashirikiana nalo."
Kiongozi huyo wa Hezbollah alisema katika hotuba iliyorushwa moja kwa moja kwenye televisheni kwamba Israel ni "nchi adui" na kwamba “lazima iondoke nchini Lebanon.”
Pia alilaumu Marekani kwa kuendelea kuwepo kwa majeshi ya Israel nchini Lebanon, akisema kuwa Marekani inabeba jukumu la hali hiyo kuendelea.
BBC





