Haukuwa mpango wangu kuzaa na Kim Kardashian – Kanye West
Eric Buyanza
April 1, 2025
Share :
Rapa mtata wa Marekani, Kanye West amedai kuwa hakuwahi kutaka kupata watoto na aliyekuwa mke wake, Kim Kardashian, lakini Mungu alikuwa na mpango tofauti.
Kanye aliyasema hayo alipokuwa kwenye mahojiano ya hivi karibuni na DJ Akademiks;
"Hilo lilikuwa kosa langu. Ninakubali. Sikutaka kupata watoto na Kim Kardashian baada ya miezi miwili ya kwanza ya kuwa naye. Lakini huo haukuwa mpango wa Mungu" alisema Rapa huyo.
Katika siku za hivi karibuni wawili hao wameingia kwenye vita kubwa ya kugombea sauti ya binti yao North kutumika kwenye muziki kama Baba yake anavyotaka huku Kim akisisitiza yeye ndiye mwenye haki kisheria ya nembo ya North.
Kanye West na Kim Kardashian, wana watoto wanne pamoja: North, Saint, Chicago, na Psalm.