Hawa hapa wachezaji 5 anaowataka Klopp kwenda nao Madrid
Eric Buyanza
April 20, 2026
Share :

Kocha mkuu wa zamani wa Liverpool, Jurgen Klopp, anataka usajili wa wachezaji watano kutoka kwa uongozi wa Real Madrid kabla ya kuwasili kwake, kulingana na ripoti.
Miamba hiyo ya Uhispania walimtimua kocha Xabi Alonso mwezi Januari baada ya kupoteza Spanish Super Cup kwa Barcelona na kisha kumpa kocha wa muda Alvaro Arbeloa ambaye naye anaonekana nafasi hiyo haimtoshi.
Kwa mujibu wa ripoti mbali mbali nchini Hispania, Klopp anahitaji saini za Rodri wa Manchester City, Alexis Mac Allister wa Liverpool na Nico Schlotterbeck wa Borussia Dortmund kama wachezaji 'wa lazima'.
Aidha Mjerumani huyo anataka pia saini ya mshambuliaji wa Juventus Kenan Yildiz na kipa wa Freiburg Noah Atubolu.
Mtaalam wa maswala ya usajili Fabrizio Romano amedokeza kuwa kuna jopo la makocha linalotakiwa na Real Madrid lakini Klopp amekuwa akitajwa sana ndani ya klabu hiyo.





