Haya hapa mashirika matano ya kijasusi yenye nguvu zaidi duniani
Eric Buyanza
May 6, 2024
Share :
Haya hapa mashirika matano ya kijasusi yenye nguvu na ushawishi mkubwa zaidi ulimwenguni;
1. SHIRIKA LA UJASUSI LA MAREKANI (CIA)
Lilianzishwa mwaka 1947, shirika bora kitaalam kuliko mashirika mengine mengi ya kimataifa na inajua mengi kuhusu matukio ya kimataifa, ina jukumu la kukusanya taarifa za kigeni, wakati mwingine hata Marekani.
2. SHIRIKA LA KIJASUSI LA ISRAEL (MOSSAD)
Mossad ilianzishwa mwaka 1949, mwaka mmoja baada ya kuundwa kwa taifa la hilo.
Israeli ni taifa la Kiyahudi katikati ya nchi tano za Kiarabu. Kwa kawaida, walihitaji wakala kama Mossad kuweka jicho ili kuwachunguza adui zake.
Ni shirika muhimu sana kwao na linafanya shughuli nyingi katika sehemu mbalimbali duniani.
3. SHIRIKA LA UJASUSI UINGEREZA (MI6)
Likiwa na makao yake makuu huko London, lilianzishwa mnamo Julai 4, 1909 na ni moja ya shirika la kijasusi lenye nguvu zaidi duniani.
4: SHIRIKA LA UJASUSI LA PAKISTAN (ISI)
ISI ndio kiini cha usalama wa nchi hiyo na makao yake makuu yako jijini Islamabad na ilianzishwa mwaka 1948.
5. SHIRIKA LA UJASUSI LA URUSI (GRU)
Shirika hili lilianzishwa mwaka 1992 baada ya kuanguka kwa Umoja wa Kisovyeti mwaka 1990.
BBC