Hazard hakuwahi kuwa na nidhamu mazoezini kama Ronaldo - Eymael
Eric Buyanza
June 12, 2024
Share :
Kipa wa zamani wa Ubelgiji, Luc Eymael, ameeleza kwa nini Eden Hazard hakufanikiwa akiwa Real Madrid.
Hazard aliwasili Santiago Bernabeu akitokea Chelsea mwaka mmoja baada ya Cristiano Ronaldo kuondoka 2018.
Alijitahidi kurudisha kiwango chake alichokuwa nacho Chelsea ikashindikana na baadae kutokana na majeraha yaliyokuwa yakimwandama aliamua kustaafu soka la kulipwa.
Akiongea na SportsBoom kwa kifupi kuhusu kushindwa kwa Hazard kufanya vizuri alipokuwa Real Madrid, Luc Eymael anasema Hazard alikuwa mchezaji mwenye kipaji kikubwa lakini hakuwahi kuwa na nidhamu katika mazoezi kama aliyokuwa nayo Ronaldo.