Headphones zinaongeza kiwango cha Bakteria masikioni
Eric Buyanza
January 12, 2024
Share :
Tunazitumia kusikilizia muziki au kusikilizia simu, matumizi ya headphones/Earbuds imekuwa ni sehemu ya maisha kwa watu wengi kila siku iitwayo leo, lakini licha ya matumizi ya mara kwa mara, watu wengi hawajui madhara ambayo yanaweza kutokea tunapozitumia kwa muda mrefu.
Utafiti uliofanyika mwaka 2008 na Chuo Kikuu cha Manipal nchini India, uligundua kuwa matumizi ya mara kwa mara ya Headphones yaliongeza idadi ya bakteria kwenye sikio.
Na mwaka 1992 utafiti katika Taasisi ya Utafiti wa Tiba ya Jeshi la Wanamaji huko Bethesda, Maryland nchini Marekani, uligundua kuwa headphones zinazotumiwa na mashirika ya ndege zilikuwa na bakteria mara 11 zaidi baada ya kuvaliwa kwa saa moja tu.
Hata hivyo kuna njia za kupunguza hatari ya maambukizi ya sikio kwa kusafisha headphones/Earbuds zako kabla ya kuzitumia kwa kitambaa chenye unyevunyevu angalau mara moja kwa wiki na pia kuepuka matumizi ya muda mrefu ili kuyapa masikio yako muda wa kupumua.