pmbet

Hesabu mpya inasoma 985, yamesalia mabao 15 tu kufikia 1,000!

Eric Buyanza

October 30, 2026
Share :

Mashine ya mabao na nahodha wa Al-Nassr, Cristiano Ronaldo, amesogeza mbele ndoto yake ya kuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya soka kufikisha mabao 1,000, baada ya kufunga mabao matatu (hat-trick) katika ushindi mnono wa 5-3 dhidi ya Al-Kholood kwenye Ligi Kuu ya Saudi Arabia (SPL).

 

Staa huyo mwenye umri wa miaka 41 alitandika mabao hayo matatu ndani ya dakika 15 tu za kipindi cha pili (dakika ya 66, 72 na 81) na kuivusha Al-Nassr kutoka kwenye sare ya 2-2 ya kipindi cha kwanza hadi kuondoka na alama tatu muhimu.

 

Hat-trick hiyo inamfanya afikishe jumla ya mabao 985 katika ngazi ya klabu na timu ya taifa, akihitaji mabao 15 tu kuweka rekodi mpya duniani.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet