pmbet

Hezbollah yathibitisha kamanda wake kufariki, mwili wake wakutwa kwenye vifusi

Eric Buyanza

August 1, 2024
Share :

Hezbollah imethibitisha kuwa mmoja wa makamanda wake wakuu wa kijeshi aliuawa katika shambulio la anga la Israel huko Beirut, nchini Lebanon.

Siku ya Jumatano jioni, kundi hilo linaloungwa mkono na Iran lilisema mwili wa Fuad Shukr ulipatikana kwenye vifusi vya jengo ambalo lilishambuliwa siku ya Jumanne.

Watu wengine wanne waliuawa katika shambulio hilo, wakiwemo watoto wawili. Awali, jeshi la Israel lilisema Shukr alikuwa akilengwa "kuuawa na ujasusi" .

Israel iliongeza kuwa shambulizi hilo lilikuwa jibu kwa shambulio la roketi ambalo liliua watu 12 katika Milima ya Golan inayokaliwa na Israel siku ya Jumamosi, ambayo Israel inasema kamanda huyo alisaidia katika masuala ya kupanga.

Hata hivyo Hezbollah imekanusha kuhusika na shambulio katika milima ya Golan. 

BBC inaripoti kuwa Fuad Shukr, ambaye alikuwa na umri wa miaka sitini, anaaminika kuwa mshauri mkuu wa kijeshi wa kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah. 

Shambulio hilo lililenga jengo moja huko Haret Hreik, sehemu ya kitongoji cha Dahiyeh cha Beirut.

Watoto waliouawa katika shambulizi hilo la anga ni mvulana wa miaka 10 na dada yake mwenye umri wa miaka sita. 
Shukr atazikwa siku ya Alhamisi, taarifa hiyo ilisema.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet