Hidaya afanya uharibifu Kisiwa cha Mafia
Eric Buyanza
May 4, 2024
Share :
Wakazi wa kisiwa cha Mafia ni miongoni mwa waliokumbwa na athari za kimbunga Hidaya kilichopiga kuanzia jana usiku na kudumu kwa saa kadhaa.
Upepo mkali ulioambatana na mvua kubwa umesababisha mafuriko, miti mikubwa ikiwamo mikorosho na minazi kudondoka kwenye makazi ya watu usiku wa manane.