pmbet

Hii combination mtaomba poo..!Pacha bora ya EURO kukiwasha tena.

Joyce Shedrack

July 19, 2024
Share :

Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Uhispania na klabu ya Athletico Bilbao Nico Williams huwenda akaungana na rafiki yake Lamine Yamal kuitumikia klabu ya Barcelona kuelekea msimu ujao wa mashindano.

 

Mkurugenzi wa Barcelona Deco amekutana na Wakala wa mchezaji huyo ili kuangalia uwezekano wa  kupata kwa haraka sahihi ya mchezaji huyo kabla hajanaswa na klabu za Uingereza ikiwemo Liverpool na Chelsea ambao wapo kwenye mawindo ya kumsaka winga huyo.

 

Nyota huyo mwenye miaka 22 alionekana kuunda safu bora ya ushambuliaji kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Uhispania akiwa pamoja na Lamine Yamal mwenye umri wa miaka 17.

Mashabiki wa Barcelona tayari wameanza kampeni na michango mbalimbali wakihakikisha kwamba Nico Williams anaitumikia nembo ya klabu hiyo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet