pmbet

Hii hapa orodha ya familia 10 tajiri zaidi duniani

Eric Buyanza

June 5, 2026
Share :

1. Familia ya Walton
Utajiri wao unakadiriwa kuwa Dola 513.4 bilioni

Familia ya Walton kwa mara nyingine tena ndiyo familia tajiri zaidi duniani.

Familia hii wanamilki maduka makubwa ya Walmart na wana jumla ya maduka 10,800 ya rejareja kote duniani.

 

2. Familia ya Al Nahyan
Ina utajiri wao unakadiriwa kuwa Dola 335.9 bilioni.
Inafanya biashara ya mafuta.

 

3. Familia ya Al Saud
Utajiri wao unakadiriwa kuwa Dola 213.6 bilioni

Familia ya kifalme ya Saudia, utajiri mkubwa wa familia hiyo unahusishwa na biashara ya mafuta.

 

4. Familia ya Al Thani
Utajiri wao unakadiriwa kuwa Dola 199.5 bilioni

Familia ya Al Thani imetawala Qatar tangu katikati ya karne ya 19.  
Utajiri wao unahusishwa na biashara ya mafuta na gesi.

 

5. Familia ya Hermès
Utajiri wao unakadiriwa kuwa Dola 184.5 bilioni

Familia ya Hermès ya Ufaransa inafanya biashara ya bidhaa za kifahari kupitia kampuni yao Hermès International.

 

6. Familia ya Koch
Utajiri wao unakadiriwa kuwa Dola 149.5 bilioni

Utajiri wao unatokana biashara nyingi mchanganyiko kama vile mafuta, Elektroniki, Kemikali, kilimo na nyingine nyingi.

 

7. Familia ya Mars
Utajiri wao unakadiriwa kuwa Dola 148.2 bilioni

Familia hii ina viwanda vikubwa vya pipi na chokoleti na pia wanafanya biashara  ya vyakula, huduma za afya na nyinginezo.

 

8. Familia ya Bettencourt Meyers
Utajiri wao unakadiriwa kuwa Dola 92.1 bilioni

Familia hii inafanya biashara ya vipodozi kupitia kampuni yao ya L'Oréal, iliyoanzishwa mwaka wa 1909.

 

9. Familia ya Ambani
Utajiri wao unakadiriwa kuwa Dola 89.2 bilioni

Familia hii kutoka nchini India inafanya biashara mbalimbali kupitia kampuni yao kubwa ya Reliance Industries Limited (RIL).  

 

10. Familia ya Wertheimer
Utajiri wao unakadiriwa kuwa Dola 88 bilioni

Familia hii kutoka Ufaransa inafanya biashara ya mitindo ya kifahari, manukato na bidhaa za urembo kupitia kampuni yao maarufu duniani ya Channel. 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet