Hii inashangaza Kombe la Dunia la Mwaka 2026 ni copy ya 2010.
Joyce Shedrack
June 16, 2026
Share :
Kuna mambo mengi yanayofanana sana kati ya Kombe la Dunia la mwaka 2026 na lile la mwaka 2010 nchini Afrika Kusini, jambo linalowashangaza mashabiki wengi wa soka.
Ingawa mashindano ya sasa ya mwaka 2026 ni makubwa kihistoria yakiwa na timu 48 katika nchi tatu wenyeji, yameiga mashindano ya mwaka 2010 kwa njia zifuatazo:

1. Mechi ya Ufunguzi Kufanana Kabisa
- Timu: Mashindano yalianza mnamo Juni 11 kwa Mexico kucheza dhidi ya Afrika Kusini. Mwaka 2010, mechi ya ufunguzi ilikuwa ni timu hizi hizi na ilichezwa tarehe hiyo hiyo ya Juni 11.
- Tofauti ya Matokeo: Mwaka 2010, mechi hiyo iliisha kwa sare ya 1-1. Mwaka 2026, Mexico ilifanikiwa kushinda 2-0 dhidi ya Afrika Kusini katika uwanja wa Estadio Azteca.
2.Msanii aliyetumbuiza kwenye ufunguzi wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010 alikuwa ni Shakira sawa kabisa na mwaka huu 2026.
3. Uhispania Kuanza Vibaya Kihistoria
- Mechi za Kwanza: Mwaka 2010, Uhispania (waliokuwa wanapewa nafasi kubwa ya kushinda) walishtua ulimwengu kwa kufungwa 1-0 na Uswisi katika mechi yao ya kwanza.
- Marudio ya 2026: Mnamo Juni 15, 2026, historia imejirudia ambapo Uhispania imeanza vibaya kwa kutoka sare ya 0-0 dhidi ya Cape Verde (ambao wanashiriki kwa mara ya kwanza). Mashabiki wengi wanakumbushia kuwa hata mwaka 2010 Uhispania ilibeba ubingwa licha ya kuanza vibaya na Wachezaji 8 wa Barcelona kuitwa Timu ya Taifa ya Uhispania kama ilivyo mwaka huu.
4.Uhispania walicheza Kombe la Dunia 2010 wakiwa Mabingwa Ulaya na walipangwa kundi H kama ilivyo mwaka huu 2026.
5. Mabadiliko Makubwa ya Mfumo
- Mifumo ya Kwanza: Mashindano ya mwaka 2010 yalikuwa ya kihistoria kwa sababu ilikuwa mara ya kwanza kwa bara la Afrika kuandaa Kombe la Dunia. Mashindano ya 2026 nayo yanaweka historia kama mashindano ya kwanza kuandaliwa na nchi tatu kwa pamoja (Marekani, Canada, na Mexico) na ya kwanza
6. 2010 Real Madrid walimaliza msimu bila kutwaa taji lolote na Morinho alijiunga rasmi na timu hiyo huku Barcelona ikichukua Kombe kla Laliga na Super Cup sawa kabisa na mwaka huu wa 2026.
7. Kazi ya Uokoaji ya Javier Aguirre
- Kocha: Kocha Javier "El Vasco" Aguirre ndiye anayeifundisha Mexico sasa hivi.
- Historia: Mwaka 2010, Aguirre aliletwa pia kuinusuru timu ya Mexico zikiwa zimebaki siku chache kabla ya Kombe la Dunia kuanza baada ya kipindi kigumu chini ya kocha Sven-Göran Eriksson. Kwa mwaka 2026, aliajiriwa tena kurekebisha timu hiyo kufuatia kuondoka kwa Jaime Lozano.





