Hii ndio sababu iliyofanya mtumwa huyu aitwe 'Calculator'
Eric Buyanza
April 26, 2024
Share :
Thomas Fuller au (Negro Tom) ni mtumwa wa kiafrika aliyezaliwa nchini Benin mwaka 1710 na kuuzwa utumwani nchini Marekani mwaka 1724 akiwa na umri wa miaka 14.
Mtumwa huyu alipewa jina "Virginia Calculator" baada ya kugundulika kuwa na uwezo wa ajabu wa kufanya mahesabu magumu kichwani bila kuandika popote.
Mfano aliulizwa kuna sekunde ngapi katika mwaka mmoja na nusu? ndani ya dakika mbili alijibu kwa usahihi kwamba ni 47,304,000.
Aliulizwa tena mtu mwenye miaka 70 na siku 17 na saa 12 ameishi kwa sekunde ngapi? Ndani ya dk moja na nusu aliweza kujibu kwa usahihi kwamba ni sekunde 2,210,500,800.
Alikuwa na uwezo wa kufanya hesabu ngumu sana kichwani na akatoa jibu sahihi akitumia muda mchache huku akiwa amezungukwa na watu wanaomuuliza maswali mengine na kumpigia kelele, lakini alikuwa na uwezo wa kujibu maswali yao kisha kurudia pale alipoishia na kutoa jibu. La hsabu aliyopewa.
Kilichowashangaza wengi ni kwamba pamoja na na kufanya mahesabu magumu hivyo hakuwahi kujua kusoma wala kuandika mpaka alipofariki mwaka 1790 akiwa na miaka 80 huko Virginia nchini Marekani.