Hii ndio sababu ya Lionl Messi kuelekeza mikono juu baada kufunga
Eric Buyanza
May 25, 2024
Share :
Hakika sote tunamfahamu Lionel Messi kama mmoja wa wachezaji bora kuwahi kutokea kwenye historia ya soka, lakini kuna vitu vingi kuhusu mchezaji huyo hatuvijui.
Moja ya vitu hivyo ni ile tabia yake pendwa ya kuelekeza mikono juu kila anapofunga bao.
Watu wengi hufikiri kwamba anamshukuru Mungu, lakini ukweli ni kwamba ishara ile ni kwa ajili ya Bibi yake marehemu Celia Oliveira.
“Ninafanya hivyo kwa sababu magoli haya ni kwa ajili ya Bibi yangu, alikuwa akinipeleka mazoezini, lakini sasa haoni mafanikio yangu”
Messi alikuwa na mapenzi makubwa na Bibi yake.