Hii ndio sababu za mtoto wa Anorld kugoma kutumia jina la baba yake
Eric Buyanza
March 21, 2024
Share :
Mtoto wa nje wa Arnold Schwarzenegger, Joseph Baena anasema licha ya kufuata nyayo za baba yake katika tasnia ya uigizaji na utunishaji wa misuli, lakini hataki kutumia jina la mwisho la dingi yake nyota wa Terminator.
Kwenye mahojiano ya hivi karibuni Joseph alinukuliwa akisema ”Ninajaribu kufanya mambo yangu kivyangu”
Joseph anatumia jina la ukoo wa mama yake..aitwae Mildred Baena, huku akijitengenezea njia yake mwenyewe huko Hollywood.
"Nadhani jambo kubwa hapa ni kwamba ninajaribu kufanya mambo yangu kivyangu...ni muhimu sana kama mwanamume kufanya mambo peke yako"
Mildred Patricia Baena mama yake Joseph alikuwa mfanyakazi wa ndani wa Arnold Schwarzenegger kabla wawili hao hawajaingia kwenye mahusiano.