Hii ni kubwa kuliko...! Simba kuzindua wiki ya Simba kwenye hifadhi ya Taifa Mikumi.
Joyce Shedrack
July 22, 2024
Share :
Bodi ya Utalii Tanzania imeingia makubaliano na klabu ya Simba kushiriki kutangaza Utalii hivyo uzinduzi wa wiki ya Simba utafanyika katika hifadhi ya Taifa Mikumi.
Siku ya jana Jumapili Julai 21, 2024 Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Imani Kajula alikutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania Ephraim Mafuru,na kukubaliana kuwa Bodi ya Utalii itakuwa ni mmoja wa wadhamini wa sherehe za Wiki ya Simba 2024.
Awali klabu ya Simba kupitia Idara ya Habari na Mawasiliano ilitangaza kufanya uzinduzi wa wiki ya Simba Mkoani Morogoro na kuwasafirisha mashabiki wake bure kupitia treni za umeme (SGR).