pmbet

Hiki hapa kiumbe cha baharini kinachoishi miaka zaidi ya 10,000

Eric Buyanza

July 24, 2026
Share :

Huenda ukawa hujawahi kusikia hili, lakini nikujuze tu kwamba kwenye dunia hii tunayoishi1 kuna mengi ya kushagaza na mojawapo linaweza kuwa hili.

Unaweza usiamini lakini 'Glass Sponge' au kwa jina la kisayansi 'Hexactinellida' ni kiumbe cha kipekee kinachoweza kuishi miaka zaidi ya 10,000.

 

Viumbe hawa wa baharini wanaishi katika kina kirefu cha bahari hasa katika Bahari ya Pasifiki ya Kaskazini na Antatika.

 

Wanasayansi wamegundua baadhi ya viumbe hawa wakiwa na umri wa hadi miaka 11,000, jambo linalowafanya kuwa viumbe wanaoishi miaka mingi zaidi duniani.

 

Miili yao imetengenezwa kwa madini ya silika na hukua kwa kasi ndogo sana katika mazingira tulivu ya chini ya maji.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet