Hispania kuumana na Ufaransa leo nusu fainali Euro
Sisti Herman
July 9, 2024
Share :
Baada ya kupumzika kwa siku tatu, leo michuano ya kombe la Mataifa Ulaya (EURO 2024) itaendelea tena katika hatua ya nusu fainali itakayowashuhudia wababe wanne waliofuzu hatua hiyo Hispania, Ufaransa, Uingereza na Uholanzi wote wakisaka tiketi ya kucheza fainali na kubeba taji.
Nusu fainali ya kwanza ambayo itaanza leo Julai 9 itawakutanisha Ufaransa waliowaondoa Ureno katika hatua ya robo fainali dhidi ya Hispania iliyowatoa wenyeji Ujerumani, mchezo huu utapigwa kwenye Uwanja wa Allianz Arena unaotumika na Bayern Munich.
Nusu fainali ya pili itapigwa kesho Julai 10 ambapo England itakutana na Uholanzi kwenye Uwanja wa Westfalenstadion katika Jiji la Dortmund, uwanja huu ukiwa ndio mkubwa zaidi ndani ya Ujerumani.
England ambayo imepita kwa penalti 5-3 mbele ya Uswisi sasa itakutana na Uholanzi iliyoipasua Uturuki kwa mabao 2-1.