Hispania Mabingwa EURO 2024, Waigaragaza Uingereza
Sisti Herman
July 14, 2024
Share :
Timu ya Taifa ya Hispania wameibuka Mabingwa wa kombe la Mataifa Ulaya (Euro 2024) baada ya kuwafunga goli 2-1 timu ya Taifa Uingereza kwenye mchezo wa fainali ya mashindano hayo uliochezwa kwenye uwanja wa Olimpia Stadion jijini Berlin nchini Ujerumani.
Magoli ya Hispania kwenye mchezo huo yamefungwa na Nico Williams dakika ya 47 na Mikel Oyarzabal dakika ya 87 huku goli la kufutia machozi la Uingereza likifungwa na Cole Palmer aliyefunga dakika ya 73.