pmbet

Hispania watamba kumstaafisha Toni Kroos kwa lazima kesho

Sisti Herman

July 4, 2024
Share :

Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Hispania Joselu amesema kuwa wanajiandaa kumstaafisha Toni Kroos kesho kwa kuwafunga na kuwatoa Ujerumani kwenye hatua ya robo fainali ya kombe la mataifa Ulaya (EURO 2024).

Hatua yoyote ya mtoano watakayoishia Ujerumani inaweza kuwa mechi ya mwisho ya kiungo huyo wa Real Madrid ambaye alitangaza kustaafu baada ya michuano ya EURO 2024 huku akiwa ameshaaga Madrid.

"Tunajiandaa kumstaafisha Kroos" alisema kwa utani Joselu kwenye mkutano na wanahabari lakini baadae Kroos alijibu kwa kusema "sidhani kama ijumaa itakuwa mechi yangu ya mwisho" kwa kujiamini huku akiwa na matumaini kuwa 'watatoboa' mbele ya Hispania.

Hispania na Ujerumani watamenyana ijumaa hii kwenye hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet