pmbet

HISTORIA KUANDIKWA: Uganda kuanza kuuza mafuta yake nje ya nchi

Eric Buyanza

September 3, 2026
Share :

Serikali ya Uganda imetangaza rasmi kuwa inatarajia kuingia kwenye orodha ya nchi zinazouza mafuta nje ya nchi kufikia mwishoni mwa mwaka huu, ikiwa ni hatua ya kihistoria baada ya miaka mingi ya maandalizi.Akizungumza wakati wa mkutano wa sekta ya nishati, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati nchini humo, Irene Batebe, amethibitisha kuwa miundombinu muhimu imekamilika kwa kiasi kikubwa na uzalishaji wa kwanza wa kibiashara unatarajiwa kuanza kabla ya mwaka huu kwisha.

 

Katika kuashiria utayari huo, Rais Yoweri Museveni amezindua rasmi jina la chapa ya mafuta ya nchi hiyo, ambayo yatatambulika kimataifa kama "Pearl Sweet". Jina hili linatokana na sifa ya mafuta hayo kuwa na kiwango kidogo cha kiberiti (low sulfur), hali inayoyafanya kuwa rahisi kusafishwa na yenye thamani kubwa katika soko la dunia.

 

Katika kuashiria utayari huo, Rais Yoweri Museveni amezindua rasmi jina la chapa ya mafuta ya nchi hiyo, ambayo yatatambulika kimataifa kama "Pearl Sweet". Jina hili linatokana na sifa ya mafuta hayo kuwa na kiwango kidogo cha 'sulfur', hali inayoyafanya kuwa rahisi kusafishwa na yenye thamani kubwa katika soko la dunia.
 

Ili kufikia soko la kimataifa, mafuta hayo ghafi yatasafirishwa kupitia Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP). Bomba hili lenye urefu wa kilomita 1,443 linajengwa kutoka nchini Uganda hadi kwenye rasi ya Chongoleani nchini Tanzania, ambako mafuta hayo yatapakiwa kwenye meli.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet