pmbet

HISTORIA! Man City washusha uzi wa tatu uliobuniwa na AI

Eric Buyanza

August 28, 2026
Share :

Klabu ya Manchester City kwa kushirikiana na kampuni ya vifaa vya michezo ya PUMA, imezindua rasmi jezi yake ya tatu (Third Kit) kwa ajili ya msimu mpya wa 2026/2027.
 

Uzinduzi huu uliofanyika jana Alhamisi ya tarehe 27 Agosti, 2026, umeweka historia ya kipekee duniani kama jezi ya kwanza ya klabu kubwa ya soka kubuniwa kwa kutumia teknolojia ya Akili Mnemba (Artificial Intelligence - AI).
 

Tofauti na jezi nyingine zilizopita, uzi huu mpya umeundwa kutokana na mawazo ya mashabiki wenyewe. Muundo wa jezi hii ulitengenezwa na shabiki wa muda mrefu wa klabu hiyo aitwaye Elliott Lacey, akitumia mfumo maalum wa kidijitali wa PUMA AI Creator.
 

Ubunifu wa Lacey uliibuka kidedea baada ya kupigiwa kura na mashabiki wengi duniani kote, ukishinda bunifu za watu wengine zaidi ya 180,000 zilizowasilishwa.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet